Wananchi wa Kata ya Manzese leo waandamana kupinga Bunge la Katiba linalo endelea

Wanacnhi  wamanzese wakinadamana wakiongozwa na Diwani wa Ubungo Mhe Boni



Wafuasi wa chadema na wananchi wa kazi wa manzese leo waliamua kuandamana nakuzunguka karibu mitaa yote ya kata ya manzese wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo mbalimbali za kuonesha kukerwa na ya nayo endelea huko bungeni dodoma kwenye bunge la katiba.
Baada ya kutembea umbali wa takribani kilomita tatu nanusu(3.5) polisi walikuja kuwa vamia na kuwasambaratisha wakiwa tayari wameshafika kwenye ofisi zao za kata (CHADEMA) na kufanya mazungumzo na vyombo mbalimbali vya habari.
Walipokuwa wanajiandaa kutawanyika ndipo polisi walio sheheni silaha za moto na mabomu ya machozi walipofika katika eneo hilo la ofisi za chadema manzese kilimani nakuanza kufyetua risasi hewani pamoja na kulipua mabomu ya machozi.
Chakufurahisha zaidi ni pale askari mmoja alipoingia ndani ya ofisi ya chadema na alipotoka ali waamuru wenzake waondke kwakuwa walio kuwa wanaanda hawakuwa wafuasi wa chedema bali walikuwa ni wahuni tu!
Huku askari wengine wakifanya kazi ya kuokota mabango ya liyo telekezwa na waanda manaji hao na kuya weka kwenye gari yao.

No comments: