MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA KILIMANJARO MH GRACE KIWELU AZINDUA MSINGI

Mjumbe wa Kamati kuu,Mwenyekiti wa ‪#‎BAWACHA‬ Mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa viti maalum Mh Grace Kiwelu amefanya uzinduzi wa misingi katika kata ya Marangu Mashariki kama muendelezo wa program ya Kanda "Tukutane kwenye misingi" katika jimbo la Vunjo....BAWACHA tukutane kwenye misingi
Msingi uliozinduliwa na Mh Grace Kiwelu

Mh Grace akipandisha Bendera kuashiria ufunguzi rasmi wa Msingi huo

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MH JOSHUA NASSARI AMEPOKEA NYUMBA MBILI ZA KISASA KUTOKA KWA WAFADHILI

Mh Joshua Nassari alipokutana na wafadhili kutoka Switzelanda kwaajili ya makabidhiano ya nyumba za Waalimu katika Shule ya Sekondari Momella
Mhe Mbunge wa arumeru Mashariki amepokea rasmi wa nyumba za kisasa za walimu (two in one), shule ya sekondari momella - kata ya ngarenayuki.

Huu ni msaada toka switzeland. Mhe Mbunge aliambatana na katibu na mkiti wa chadema Wilaya , madiwani wa ngabobo, Uwiro na mwenyekiti wa kijiji cha Olkung'wado mzee Malimwengu (CDM) ambaye pia amekuwa msimamizi mkuu wa mradi huu.

Mhe Nassari pia aliwakaribisha wahisani hawa nyumbani Kwake Kwa Chakula cha mchana ambapo walikubaliana kuendeleza ushirikiano.
"Nimeshiriki kazi za maendeleo MERU tangu mwaka 1994 lakini hakuna Mbunge hata mmoja aliyewahi kujali au kukutana na sisi, wewe ni wa kwanza kufanya hivyo" alisema Emily Karafiat, mwakikishi wa wahisani.





ILI MAONYESHO YA WAKULIMA NANE NANE YAWE YENYE TIJA WAANDAAJI WATAKIWA WAIGE NCHI JIRANI

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh Feeman Mbowe Akiwa na Mwenyekiti wa Kanda Na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa (Katikati) Na Meya Wa jiji la Arusha Mh Kalist Lazaro wakiwa katika viwanja vya  Nane Nane,

Ili maonyesho ya wakulima Nane Nane yawe yenye tija na kuvutia nchi za nje kushiriki maonyesho haya, haina budi waratibu na waandaaji kutoka nje ya Tanzania na kuiga ni vipi wenzetu wanaandaa maonyesho yao.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ((CHADEM), Mhe. Freeman A. Mbowe alipotembelea maonyesho ya wakulima Nane Nane katika viwanja vya (TASO), Themi Njiro jijini Arusha,leo Jumane  09/08/2016.

Mhe. Mbowe amesema ni vyema sasa ikaachwa kufanywa maonyesho hayo kimazoea na kuonekana kama gulio, bali miundo mbinu iboreshwe ikiwemo na utaratibu wa wakulima kuonyesha shughuli zao pamoja na kuboresha usafi wa mazingira katika viwanja.

"Ni vyema miundombinu ikaboreshwa ili kuvutia wakulima wakubwa wa nje kushiriki maonyesho haya na kubadilishana mawazo, tutembee Kenya,Uganda, Zimbabwe na kwingineko tuone sio kwamba nadharau maonyesho haya ila inatakiwa tukifunze kwa wenzetu wanavyofanya " amesema Mhe. Mbowe.

Unaweza ukajenga sehemu ambayo watakaa wakulima wakigeni tu, mfumo mzuri wa kuonyesha bidhaa zao (display) zenye kuvutia, unatenga sehemu za wakulima wadogo wadogo, sehemu ya migahawa inakuwa ikijitegemea inakuwa ni sehemu ya kulisha washiriki wa maonyesho hayo.

Mhe. Mbowe ametaka wataalam washirikishwe zikiwemo sekta binafsi, waache kushirikisha wanasiasa,wabunge, wakuu wa wilaya n.k, mtu hajawahi kuwa hata na bustani yupo kwenye bodi, amehoji umewahi kusikia wapi?

Lazima washirikishwe wataalam, ambao watasaidia maonyesho ya Nane Nane kukuwa, hii moja ya chanzo kikubwa sana cha mapato kwa jiji la Arusha na sehemu nyingine ambayo maonyesho haya hufanyika.

Mbowe amemtaka Meya wa jiji la Arusha, Mhe. Kalist Lazaro na wenzake waende Kenya wachukue ujuzi wa jinsi ya kufanya Nane Nane kuwa yenye mvuto zaidi ili yazidi kukuwa badala ya kushuka.

Pembejeo zote zinazohusu kilimo ziwepo, elimu ya kutosha watuvkushiriki maonyesho kutoa elimu na kujifunza badala ya kwenda na kukaa kwenye mabanda ya nyama choma siku nzima.

Wakulima wafundishwe jinsi kuandaa mbegu, kupanda, kutunza shamba, kuvuna, kutafuta masoko, kuyapa thamani mazao ya kuleta maendeleo kwa kukuza uchumi wa kila mkulima na taifa kwa ujumla.