JOSHUA NASSARI AKIFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA WANANCHI WAKE

Joshua Nassari Anasema -Kazi za Ujenzi wa chanzo kipya cha Maji ya kunwagilia yaani Intake kwa kijiji cha Karangai kata ya Kikwe - Arumeru Mashariki. Tuliazna asubuhi saa tatu mpaka jioni saa kumi na mbili. 
Lengo ni maji yafike kuokoa mazao yanayotaka kukakuka mashambani. Nilijitolea kulipia malori matatu kwa siku nzima kufanya kazi hii na nyaya maalum (chain link) za kufungia/kujengea Mawe kwenye chanzo. Tulichinja mbuzi tukapika ugali site na kupiga kazi ma vijana zaidi ya 300.
Tunawashukuru pia kina mama waliokuja kututia Moyo.
Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu





Joshua Nassari Na wananchi wake wakiwa Kazini

Joshua Nassari Na wananchi wake wakiwa Kazini

No comments: