Jaji Joseph Sinde Warioba |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba imeondoa mambo manne muhimu yaliyokuwa kiini cha kupata Katiba ya mageuzi. Akiyataja mambo hayo muhimu ambayo ni maadili ya viongozi wa umma, madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka na muungano. “Tutakutana mtaani. Tume tutaendelea kutetea rasimu yetu na wao wawaeleze wananchi kwa nini wameondoa maoni yao yaliyokuwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba,” aliongeza kwa ufafanuzi Jaji Warioba.
Akizungumza
katika maadhimisho ya miaka 19 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC) Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema rasimu
hiyo inatofautiana kwa kiasi kikubwa na rasimu iliyotolewa na tume hiyo
Desemba mwaka jana. “Sina
hakika kama tutapata Katiba Mpya labda Katiba iliyoboreshwa. Rasimu au
Katiba itakayopendekezwa na Bunge Maalumu haitapigiwa kura hadi 2016.
Sina hakika kama kura hiyo itapigwa kwa kuwa hakuna maridhiano hasa
kuhusu muungano, rasimu hiyo itaanza kupingwa tangu siku ya kutolewa
kwake,” alisema. Aliongeza,
“Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka kesho Katiba Mpya itakuwa agenda,
na agenda hiyo inaweza kuigawa nchi. Kuna uwezekano mkubwa kwamba mwaka
2016 badala ya kupiga kura mchakato ukaanza upya.”
Jumatano
wiki hii Mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew Chenge aliwasilisha rasimu
hiyo bungeni na kueleza kuwa kamati yake imefuta ibara 28 zilizokuwa
katika rasimu ya Jaji Warioba na kuacha ibara 47, kuongeza ibara 42 na
kurekebisha ibara 186. Alisema
rasimu hiyo ina sura mpya mbili ambazo ni Mamlaka na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na nyingine inayohusu Ardhi, Maliasili na Mazingira
ambayo haikuwekwa katika rasimu ya Warioba kwa kuwa si mambo ya
muungano. Rasimu
hiyo ilirejesha muundo wa Serikali mbili kama ilivyo sasa na kutupilia
mbali muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba.
Huku
akiwa makini, Jaji Warioba ambaye alitumia saa 1:02 kufafanua umuhimu
wa mambo manne yaliyoachwa katika rasimu iliyotolewa na Bunge la Katiba,
alisema hivi sasa wajumbe wa Bunge la Katiba wana msemo wao kuwa
“Warioba ni shida”, kufafanua kuwa watakapomaliza vikao vya Bunge hilo
Oktoba 4, mwaka huu na kurejea mtaani walipo wananchi ndiyo watajua nani
ni ‘shida’, kati yake na wao. Akizungumzia
kitendo cha Bunge hilo kubadili kanuni ili kuruhusu wajumbe wake kupiga
kura za kupitisha rasimu hiyo kwa baruapepe (e-mail) na nukushi (fax)
wakiwa nje ya nchi, Jaji Warioba alisema, “Utaratibu huu hauwezi
kutuletea Katiba ya maridhiano. Hata mimi nimeanza kukata tamaa.”
Huku
akishangiliwa kila mara na mamia ya watu waliohudhuria kongamano hilo,
wakiwamo wasomi na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Warioba alisema kila mjumbe wa tume hiyo alikuwa na mawazo
yake juu ya Katiba, lakini waliweka kando mawazo yao baada ya kusikia
kauli za Watanzania juu ya Katiba wanayoitaka. Katika
maadhimisho hayo, Jaji Warioba pia alizindua kitabu cha marehemu Dk
Sengondo Mvungi kiitwacho ‘Mvungi anapumua Katiba’. Dk Mvungi aliyekuwa
mjumbe wa Tume ya Katiba na mmoja wa waanzilishi wa LHRC, alifariki
dunia mwaka jana nchini Afrika Kusini alikopelekwa kutibiwa baada ya
kujeruhiwa na majambazi akiwa nyumbani kwake.
Maadili ya Viongozi wa umma
Kuhusu
maadili ya viongozi wa umma alisema, “Wananchi walitoa maoni mazito
kuhusu maadili ndani ya jamii na maadili ya viongozi. Kutokana na maoni
ya wananchi Tume iliimarisha misingi mikuu ya taifa iliyo katika
Utangulizi wa Rasimu. Misingi iliyo katika katiba ya sasa ni uhuru,
haki, udugu na amani.” Alisema
kutokana na maoni ya wananchi misingi mipya iliongezwa ambayo ni; utu,
usawa, umoja na mshikamano na kwamba wananchi pia walipendekeza tunu za
taifa ziwekwe kwenye katiba ambazo ni utu, uzalendo, uadilifu, umoja,
uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa (Kiswahili ). “Bunge
Maalumu limeondoa uadilifu, uzalendo, umoja, uwazi, na uwajibikaji
kutoka kwenye orodha ya tunu za taifa na kuziweka kwenye misingi ya
utawala bora. Kila Mtanzania anatakiwa awe mzalendo, kila Mtanzania
anatakiwa kuwa mwadilifu, kila Mtanzania anatakiwa aenzi umoja.
Inakuwaje mambo haya yahusu utawala tu?” alihoji.
Alisema
tunu za taifa ndiyo msingi wa utamaduni na maadili ya taifa, kwamba
mwelekeo wa taifa utategemea jinsi wananchi wanavyoenzi misingi mikuu na
tunu. Aliponda
kitendo cha Bunge la Katiba kutoweka miiko ya uongozi kwenye Katiba
wakati kila siku viongozi wanalalamika juu ya rushwa na ufisadi, pamoja
na fedha za umma kuwekwa kwenye akaunti za benki nje ya nchi. “Katika
bara la Afrika, nchi kama Afrika Kusini, Namibia na Kenya zimeweka
misingi ya maadili na miiko katika Katiba. Hapa kwetu sheria tulizonazo
haziwezi kupambana na rushwa na ufisadi. Sijui kwa nini Bunge la Katiba
wameondoa hili,” alisema.
Madaraka ya Wananchi
Jaji
Warioba alipinga kitendo cha Bunge la Katiba kuondoa kipengele cha
wananchi kuwa na madaraka ya kumwondoa mbunge wao kama hawaridhishwi na
uwakilishi wake bungeni, mbunge kutokuwa waziri ili aweze kuwawakilisha
vizuri na ukomo wa mbunge kuwa vipindi vitatu . “Bunge
lina kanuni za kuwawajibisha wabunge na wananchi nao wanapenda kuwa na
madaraka hayo. Vyama vya siasa vina madaraka ya kuwaondoa wabunge wao
katikati ya kipindi. Wananchi nao wanataka watumie madaraka yao,”
alisema.
Mgawanyo wa madaraka
Akizungumzia
mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya Bunge, Serikali na Mahakama,
alisema pendekezo lao la kumwondoa rais na mawaziri kutoka kwenye Bunge
linakataliwa kwa sababu nchi imezoea mfumo wa kibunge kama ilivyo kwa
nchi nyingi za jumuiya ya madola. “Siyo
kweli kwamba mfumo wetu ni wa kibunge. Kwenye mfumo wa kibunge mkuu wa
nchi hana madaraka ya utendaji. Madaraka hayo yako mikononi mwa Waziri
Mkuu ambaye ni mbunge. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Uingereza, India, Canada,
Australia, New Zealand,” alisema. Akitolea
mfano mwingiliano huo alisema wakati wa kutunga Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, bunge lilitunga sheria lakini baadaye Rais alifanya mazungumzo
na watu nje ya bunge na baadaye bunge likalazimika kubadili uamuzi.
“Tanzania
ina mfumo wa urais ambapo rais ni mkuu wa nchi, mtendaji mkuu na amiri
jeshi mkuu. Rais na mawaziri wake kuwa sehemu ya bunge ni kuchanganya
mamlaka. Hali hii inafanya Serikali kuingilia mamlaka ya bunge na pia
bunge kuingilia mamlaka ya Serikali,” alisema. Aliongeza,
“Nchi nyingi zimebadili Katiba zao ili kutenganisha madaraka ya
mihimili. Jirani zetu wa Msumbiji na Kenya wamefanya hivyo. Kenya
imefanya hivyo na sababu zao zinafanana kabisa na zile ambazo wananchi
wa Tanzania walitoa.”
Muungano
Huku
akitaja kero 20 za muungano, 11 za Zanzibar na 10 za Tanzania Bara
zilizotajwa na wananchi wakati wa kukusanya maoni, Jaji Warioba alisema,
“Ingawa Rasimu ya Bunge Maalumu limerudisha madaraka ya rais kuigawa
nchi hiyo peke yake haitoshi. Mambo haya ni magumu kubadilika kwa upande
wa Zanzibar.” Aliongeza
kuwa ili kufanya mabadiliko kwenye Katiba ya Zanzibar ni lazima
mabadiliko yapitishwe kwa theluthi mbili au zaidi ya Wawakilishi.
Mwananchi
Dar es Salaam. Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema
Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu
la Katiba imeondoa mambo manne muhimu yaliyokuwa kiini cha kupata
Katiba ya mageuzi. Akiyataja
mambo hayo muhimu ambayo ni maadili ya viongozi wa umma, madaraka ya
wananchi, mgawanyo wa madaraka na muungano. “Tutakutana mtaani. Tume
tutaendelea kutetea rasimu yetu na wao wawaeleze wananchi kwa nini
wameondoa maoni yao yaliyokuwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba,”
aliongeza kwa ufafanuzi Jaji Warioba.

Muungano Huku
akitaja kero 20 za muungano, 11 za Zanzibar na 10 za Tanzania Bara
zilizotajwa na wananchi wakati wa kukusanya maoni, Jaji Warioba alisema,
“Ingawa Rasimu ya Bunge Maalumu limerudisha madaraka ya rais kuigawa
nchi hiyo peke yake haitoshi. Mambo haya ni magumu kubadilika kwa upande
wa Zanzibar.” Aliongeza
kuwa ili kufanya mabadiliko kwenye Katiba ya Zanzibar ni lazima
mabadiliko yapitishwe kwa theluthi mbili au zaidi ya Wawakilishi.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment