Akizungumza na vyombo vya habari, mwenyekiti wa chama hicho mkoani
Arusha Bw Amani Golugwa amesema anashangazwa na hatua ya polisi ya
kusambaza askari wake kila kona kudhibiti maandamano hayo kabla ya chama
hicho kuanza maandamano hatua ambayo amezidi kusisitiza kuwa ni ushindi
wa Chadema kwani hawakuwa na agenda ya kundamana bali walikuwa na machakato wa maandalizi ya maandamano hayo yasiyokuwa na kikomo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la jiji la Arusha Bw Godbles Lema
aliyeonekana kuwa karibu na kikundi cha polisi hao waliokuwa doria
amesema amemuamua kukaa karibu na kikundi cha askari wa kutuliza ghasia
kumlinda na pia kuepusha kile kinachodaiwa kama muwaandaji wa maandamano
hayo na kusisitiza kuwa bado azma ya kufanyika kwa maandamano hayo ipo
kwani wamebuni mbinu mpya ya kuwasilisha ujumbe wao maandmano hayo
yakiwemo ya polisi kudhibiti maeneo yote ya jiji hilo.
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani Arusha Bw Liberatus Sabas
akizungumza kwa ufupi kwa njia ya simu amekanusha kudai kuwepo kwa
askari hao ni sehemu ya ulinzi na ndo maana hakuna mtu yeyote
aliyekamatwa, huku baadhi ya wananchi wakiitaka serikali kuruhusu
maandamano hayo kwa amani.
No comments:
Post a Comment