Jaji Warioba azungumzia BMK lilivyochakachua maoni ya Wananchi akizindua kitabu cha Dk Mvungi 'Breathing the Constitution'


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba lilivyochakachua maoni ya wananchi wakati wa hafla ya kutimiza 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu jijini Dar es Salaam.

Katika maadhimisho ya 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, amesema wameamua kumuenzi Dk. Mvungi katika siku ya Haki za Binadamu kwa kumwandikia kitabu, kwa kuwa miaka 19 akiwa na rafiki yake Dk. Ringo Tenga walipokea hati ya usajili wa kituo hicho.

Maadhimisho hayo yamempa heshima Jaji Joseph Sinde Warioba ya kuzindua kitabu kinachohusu maisha na kazi za kisheria alizopata kuzifanya na kuziamini Dk. Sengodo Mvungi, kinachoitwa ‘Breathing Constitution’, kwa tafsiri nyepesi, Dk. Mvungi ‘anapumua Katiba’.

Dk. Kijo Bisimba, alisema kituo hicho kilipata pumzi ya kwanza Dk. Mvungi akiwa Mkurungenzi wa muda na kuandaa mkutano wa kwanza wa bodi ya wakurugenzi na kukabidhi shirika lililokuwa na usajili wa kudumu.

Mkurugenzi huyo, alisema watamkumbuka Dk. Mvungi katika mambo mengi pale wanaposherehekea maisha na umri wa kituo chao alichowezesha kuanzishwa na kubwa kuliko lote, hoja yake ya uwepo wa Katiba mpya.


“Katika sherehe yetu hii ya kupevuka na ya utu uzima, mwaka jana Septemba 26, Dk.. Mvungi alikuja na furaha sana…alisema ilibidi aondoke kidogo kwenye kazi nyeti aliyokuwa nayo katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili tu awepo nasi, na kusema hata atingwe na kazi kiasi gani hawezi

kuacha kuwepo katika harusi ya mwanae,” alisema na kuongeza: “Tumeona na imekuwa ni vizuri kwetu kuona kazi aliyoifanya na hatua iliyofikia siku mbili kabla ya leo …Bunge Maalum la Katiba ambalo Dk. Mvungi alilitaja kuwa ndiyo Katiba yenyewe, wiki hii limetoa rasimu nyingine ya Katiba ambayo ndiyo itakayojadiliwa kuwa Katiba. Je angekuwepo pamoja nasi angesema nini kuhusiana na rasimu,” alihoji Dk. Kejo Bisimba

Alisema Dk. Mvungi leo hii angekuwepo, angeshangaa zaidi kuona jinsi ambavyo mchakato wenyewe ulivyokiuka kabisa taratibu zote zilizowekwa kisheria na kuchukua utaratibu mpya na kanuni zinazobadilishwa mara kwa mara ili kukidhi matakwa yao na kukimbiza kura ili kupata akidi.

Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wakiwa katika mkutano huo.


Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia (kulia).

Ndimara Tegambwage (katikati), kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Katika salamu zake, Mwakilishi wa familia ya Dk. Mvungi, aliyejitambulisha kwa jina la Adrian Mvungi, aliwataka wana LHCR kuendeleza yale yote yaliyoachwa na baba yake, ambaye alisema alikuwa ni mtetezi wa wanyonge na nguzo ya haki za binadamu.

“Familia inatoa shukrani kwenu LHCR kwa kuona kuwa Dk. Mvungi alitoa mchango mkubwa katika taifa hili hata kuratibu na kutunga kitabu chake …tujiulize kwa pamoja yaliyotokea mpaka anafariki na yanayoendelea, tunajiuliza baba yetu yuko wapi.

“Ondoeni woga katika kutetea haki za binadamu na endelezeni mazuri yote ya Dk. Mvungi aliyoyafanya, kwa sababu wamemuua mwili tu roho yake inaendelea kufanya kazi kwa kuwa mtu/watu dhaifu hulipa kisasi… lakini mtu/watu imara, husamehe,” alisema.

Mwakilishi wa Chama alichokuwepo Dk. Mvungi, NCCR-Mageuzi, Mwenyekiti wake James Mbatia, alisema wataendelea kuyaenzi yote walioasisiwa zikiwamo fikra na michango yake katika chama hicho na hasa kuhusu Katiba.

“Tunakumbukumbu ya mambo mengi aliyotuachia Dk. Mvungi hasa Katiba, hata siku mbili kabla ya kufa alituambia mengi kuhusu Katiba … nitayarudia maneno yangu niliyoyasema siku tunamuaga katika viwanja vya Karimjee Novemba 11 mwaka jana kwamba, tutahakikisha taifa linapata Katiba ya maridhiano ya watu wote na siyo ya upande mmoja,” alisema Mbatia.

Naye Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Perepetua Kessy kwa niaba ya wanawake waliokuwepo ukumbini, alisema atamkumbuka Dk. Mvungi kwa kuwaweka mbele wanawake kuwa wana haki sawa na wanaume, hata kusimamia hoja ya uwakilishi wa nusu kwa nusu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk. Helen Kijo Bisimba (kushoto), Askofu Elinaza Sendoro na Prof. Chris Maina (kulia).

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizindua kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na Dk. Sengondo Mvungi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk. Helen Kijo Bisimba (kushoto), akionyesha kitabu cha Breathing the Constitution. Kulia ni Askofu Elinaza Sendoro.

No comments: