Baraza la
Wanawake wa Chadema (Bawacha) limetangaza maandamano kwenda Ikulu kumuomba Rais
Jakaya Kikwete asikubali kutia saini Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwapo
itapitishwa na Bunge.
Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee alisema jana kwamba maandamano hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo, baada ya maandalizi yatakayofanyika kwa siku saba kuanzia jana kukamilika. |
Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe,
alisema baraza hilo limeamua kuitisha maandamano hayo ili kuwakilisha kilio cha
wanawake ambao ndiyo waathirika wa kwanza pale nchi inapokuwa katika mfumo usio
wa haki.
Alivitaka vyombo vya dola hasa
polisi kujitokeza kuwasindikiza na kuandamana nao kwa kuwa nao ni miongoni mwa
Watanzania ambao wataathiriwa na uamuzi usiolenga kujenga umoja wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment