Baraza la vijana wa CHADEMA


(BAVICHA ) Leo wanatarajia kuzindua Matawi zaidi ya Matano,katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni.Akizungumza asubuhi hii msemaji wa Baraza,ambae pia ni Mratibu wa Uhamasishaji BAVICHA Taifa Bw.Edward Simbeye amesema,uzinduzi wa Matawi hayo ni chachu kubwa kwao kama Viongozi wa BAVICHA kuendelea kuimarisha mshikamano wa kiutendaji baina yao na Wanafunzi wa Vyuo vikuu vyote nchini.

Matawi hayo yata zinduliwa na Katibu Mkuu wa BAVICHA Taifa JULIUS MWITA,shughuli ambayo inatajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 800 kutoka vyuo tofauti Mkoani Dar es Salaama.

Msafara huo Katibu Mkuu wa BAVICHA ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA bara na Muweka hazina wa Baraza hilo Bi.Evelyne Meena.

No comments: