CHAMA CHA DEMOKRASIA NA
MAENDELEO – CHADEMA
KANDA YA KASKAZINI
(Tanga, Kilimanjaro,
Arusha & Manyara)
MPANGO WA MABARAZA WA KUELEKEA
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015
UTANGULIZI:
Maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndani ya
chama katika ngazi mbalimbali yanaendelea kwa kasi kubwa. Wanachama wengi
katika hatua hii wameonyesha nia ya kutaka kugombea kupitia CHADEMA. Hii ni
hali njema na ambayo inaendelea kutoa wajibu mkubwa unaohitaji kuthibitisha
ukomavu wa viongozi wa chama katika kukabiliana na kukua kwa chama huku chama
kikiendelea kusimamia malengo ya msingi pasipo na kuruhusu migogoro wala
chokochoko zozote.
Mpango huu unaendana sambamba na kuendelea kuitaka
serikali kwa gharama yoyote ile kuwa uchaguzi mkuu lazima ufanyike mwaka huu,
hivyo suala la uandikishwaji katika mfumo wa BVR lazima lifanyike na lipewe
kipaumbele cha kipekee.
Pamoja na malengo mengine, mpango huu una lengo la
kufanya kazi ya siasa ikilenga kituo cha kupiga kura na mpiga kura kwa ukaribu
zaidi “Micro Targeting” baada ya kuwa ameshajiandikisha kupiga kura.
MABARAZA YA
CHAMA: WANAWAKE, VIJANA & WAZEE
Mabaraza ya chama ni vyema yajitambue na kujielewa
wajibu mkubwa walio nao sasa wa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya
kuelekea uchaguzi mkuu. Kupitia programu hii, RIKA za makundi haya
zitashirikishwa kwenye maeneo yao husika ya makazi kufanya kazi ya siasa
kuelekea uchaguzi mkuu.
Uhalisi wa Mabaraza ya chama kwenye maeneo mengi
ya makazi, yaani uratibu wa makundi RIKA kichama haupo kwa nguvu ya kiridhisha,
ingawa fursa ya uratibu ipo sana kwa upande wetu.
Mfano mpango
huu kwa Mkoa wa Arusha na Jimbo la Arusha Mjini:
Idadi
ya watu Mkoa wa Arusha (Sensa ya mwaka 2012)
Jumla Wanaume Wanawake % Ongezeko (2002 – 2012)
1,694,310 821,282 873,028
2.7
Arusha Mjini: (Sensa ya mwaka 2012)
Jumla Wanaume Wanawake
416,442 199,524 216,918
Makadirio
ya wapiga kura (kwa ongezeko la kisensa la watu kuhamia na la watu kufikia umri
wa kupiga kura)
Arusha Mjini:
Jumla Wanaume Wanawake
270,543 129,863 140,680
KUELEKEA
UCHAGUZI MKUU:
Katika maandilizi ya kuelekea uchaguzi mkuu, suala
la kuandikishwa wapiga kura ni jambo la muhimu sana. Hivyo chama lazima tuwe na
mpango maalumu wa kufanya ili kuhakikisha kuwa tunao watu walioandikishwa na
ambao watatupigia kura.
Mabaraza kwa maana hii, yatatakiwa kufanya kazi
kubwa kwenye makundi RIKA yao kuhakikisha kuwa VIJANA, WAZEE na WANAWAKE
wanajiandikisha ili wakati wa uchaguzi waweze kwenda kupiga kura.
MPANGO
WENYEWE: MPANGO BARAZA -75 ( MB-75 )
Kila BARAZA kwenye MTAA au KITONGOJI litatakiwa
kusajili wanachama wa RIKA lake 25.
Kazi hii itafanywa, kwa kuratibiwa na kusimamiwa
na Baraza husika kwenye ngazi ya KATA kwa kutekelezwa kwenye mtaa au kitongoji.
Kila Kata itaandikisha kundi rika la watu 25. Kutahitajika ushirikiano wa
karibu sana kutoka kwa wenyeviti wa mitaa/vijiji na vitongoji katika kutekeleza
mpango huu hasa kwenye kuweka kumbukumbu sahihi ya wajumbe walioandikishwa wa
mabaraza.
Watu hawa wa Mabaraza watakaotekeleza mpango huu
wataitwa “MB Kamanda”
Watu hawa
25 watakuwa na wajibu ufuatao:
- Kuhamasisha na kuhakikisha angalau si chini ya watu 10 kwenda kujiandikisha kupiga kura (kwa mfumo wa BVR) kwenye eneo lake la mtaa au kitongoji chake na kupata ushahidi wa kitambulisha cha kila mtu kujiandikisha
- Kuweka rekodi ya majina, namba za simu na kitambulisho namba za watu hawa KUMI waliojiandikisha kupiga kura
- Taarifa hii (nakala) aipeleke ngazi ya kata ambayo itafikishwa kwa Mwenyekiti wa Baraza husika kwa ngazi ya Jimbo.
- Mwenyekiti wa Jimbo wa Baraza husika atapeleka majina haya na namba za simu kwa Kampeni meneja wa jimbo husika ka ajili ya kuendeleza mawasiliano na watu hawa waliojiandikisha. Mawasiliano na watu hawa itakuwa kwa njia ya meseji kwa mfumo wa “bulk sms”.
- MB Kamanda atahakikisha kuwa wakati wa kampeni anamhamasisha kila aliyemuandikisha kwenye listi ama kwenda kwenye mikutano ya hadhara au kumpelekea taarifa sahihi za wagombea wetu wa udiwani, Ubunge na Urais
- MB Kamanda atahakikisha siku ya kupiga kura anamkumbusha na kuhakikisha watu aliowaandikisha kwenda kupiga kura wanakwenda kupiga na wanawapigia kura wagombea wetu.
- Uongozi wa Jimbo wa Mabaraza husika wataandaa fomu na maboresho watakayoyaona yanafaa kwa ajili ya kuboresha mpango huu.
FOMULA YA NAMBA
YA KIMKAKATI kwa kutumia mfano wa jimbo la Arusha Mjini:
Mpango Baraza Watu: 75
Kila mmoja KUPATA watu 10 (zaidi ya idadi hii ni bora zaidi
lakini isizidi 20) kujiandikisha kupiga kura na kwenda kupiga kura
Mitaa 154
Idadi: 75 X 10 X 154 Jumla Watu 115,500
Idadi hii ni sawa na asilimia 43 ya jumla ya idadi
ya wapiga kura wa Jimbo la Arusha Mjini inayokadiriwa ya wapiga kura 270,543
Hivyo mabaraza yanaweza kuchangia asilimia 43 ya
ushindi wa CHADEMA iwapo yatafanya huu mkakati.
Maantiki ya mpango huu ni kuwa, mabaraza yakifanya
kazi hii vizuri na kwa umahiri mkubwa, mafanikio yafuatayo yatapatikana;
- Mpango utaleta uhai wa kiutendaji kwenye mabaraza ya chama kwenye ngazi zote mpaka ngazi za chini.
- Mpango utakipa chama uhakika wa kura mapema kwa zaidi ya 40% kwa kuwa na uhakika wa watu waliojiandikisha na ambao watatupigia kura za ushindi
- Mpango utayaweka mabaraza kwenye utendaji na hivyo kuleta mwamko na hamasa ya makundi RIKI kushiriki kwenye siasa kipindi hiki cha uchaguzi
- Mpango utaweza kusaidia kupata mawakala kwenye vituo vya kura siku ya uchaguzi na hivyo kuondoa tatizo la kusaka mawakala dakika za mwisho. Hii itaendana na kuanza kufanya mapema maandalizi ya mafunzo kwa mawakala.
- Mpango utakiimarisha chama kwenye ngazi za chini kabisa za uratibu za kichama yaani misingi.
MUHIMU:
Mpango huu, unahitaji ubunifu sana wakati wa
utekelezaji wake. Viongozi kwenye ngazi ya Jimbo na Kata wanatarajiwa kuwasadia
watendaji (MB Kamanda) katika kuwapa namna nyepesi ya kufanya katika kuwatafuta
watu 10, kuweka rekodi ya watu hao 10 sambamba na namna au mfumo mzuri wa
kuhakikisha taarifa za watu hao 10 zinafika kwa kiongozi wa jimbo wa baraza
husika na hatimaye kwa meneja wa kampeni wa jimbo.
*****************************MPANGO BARAZA – 75******************************
************************************MB–75************************************
Amani Sam
Golugwa
KATIBU WA
KANDA – KASKAZINI
No comments:
Post a Comment