Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mh Helga Mchovu akiongea na wafanya biashara wa Soko la kwasadala |
Akiwahutubia wananchi na wafanyabiashara wa soko la KWA SADALA leo, mh Helga amewaeleza wafanyabiashara hao kwamba serikali inayoongozwa na CHADEMA katika Halmashauri hiyo haina lengo la kuwanyanyasa wananchi kupitia kodi za kero hasa kwa wafanyabiashara wa kipato cha chini na wakulima.
Hivyo amewasihi wafanyabiaahara hao kulipa km ilivyo ada ushuru katika soko hilo km ilivyopitishwa na Halmashauri ili serikali iweze kuleta mapato yatakayokwenda katika shughuli za maendeleo km elimu, afya,maji nk.
Mh Helga ameagiza wale wote wanaowanyanyasa wananchi kwenye suala la ushuru pamoja na kuwatolea lugha zisizofaa wachukuliwe hatua mara moja pamoja kuondolewa kabisa kazini.
Wakizungumza kwenye mkutano huo baadhi ya wafanyabiashara walisema kero kubwa katika hilo soko ni pamoja na kuvuja kwa paa la hilo soko, kukosekana kwa maji ya uhakika, vyoo bora, soko kutokuwa na taa na ulinzi madhubuti wa soko hasa nyakati za usiku.
Akijibu hoja hizo mh Helga amesema nyingine zipo kwa hatua za umaliziaji na nyingine amezichukua kwa ajili ya kwenda kuzifanyia kazi kwa mujibu wa taratibu.
Hivyo akawaasa wananchi waendelee kufanya biashara kwa kulipa ushuru na km kuna matatizo yoyote apelekewe ofisini au kwa kupigiwa simu moja kwa moja ili kukabiliana na changamoto kwa wakati.
Baada ya hapo kwa kauli moja wafanyabiashara hao wamekubali kwa kauli moja kulipa ushuru huo na kumshukuru mwenyekiti kwa kuheshimu ahadi aliyoitoa ya kuja kuzungumza nao.
Mfanya Biashara akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mh Helga mchovu |
No comments:
Post a Comment