MBOWE AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MIFUKO CHA HARSHO KILICHOPO HAI




Mbunge wa jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama wa Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe, Jana Jumatano 20/07/2016 amefanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza mifuko cha Harsho kilichopo katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Mbowe amempongeza Mkurugenzi wa kiwanda hiko Ndugu. Harold Shoo, kwa ujasiri na maamuzi ya kuweka kiwanda hiko katika jimbo la Hai, uwepo wa kiwanda hiko katika jimbo la Hai ambalo Mbunge wake ni Mhe. Mbowe, inasaidia kuongeza fursa za ajira kwa wakazi wa Hai na maeneo jirani.

Serikali inakusanya kodi kutokana na kiwanda hiki kuwepo hapa, inakusanya kodi kutokana na bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha Harsho, hivyo kuifanya Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake katika kuboresha elimu, huduma za afya, kujenga miundombinu salama, kuhakikisha maji salama yanapatikana, kubuni miradi endelevu ambayo itanufaisha jimbo la Hai katika kukuza uchumi imara na kupambana na umasikini miongoni mwa wananchi.

Akiongea Mkurugenzi wa kiwanda hiko, Bw. Harold Shoo amemshukuru sana Mbunge wa jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe kwa kuwatembelea na kumtaka kushirikiana pamoja kuleta maendeleo Hai, amemuahidi kumpa ushirikiano wakati wowote atakapohitaji, milango yake ipo wazi.



No comments: