ZIARA YA KATIBU WA KANDA MHE AMANI GOLUGWA -WILAYA YA BABATI TAR 04/03/2015

Katibu wa Mkoa wa Manyara Mhe Martin Mayaya akifungua kikao cha Wilaya ya Babati, Katikati ni Katibu wa Kanda Mhe Amani Golugwa akifuatiwa na Mwenyekiti wa Wilaya Babati  Mhe Edward Mollel na Mwenyekiti wa Mkoa wa Manyara Mhe Laurent Tara

Wajumbe wa wilaya ya Babati waliofika katika ofisi za Jimbo la Babati Mjini ambako kikao kilifanyikia



Katibu wa Kanda Mhe Amani Golugwa Akiwakumbusha Viongozi wajibu wao katika ujenzi wa Chama ,Pia amewataka Viongozi kufanya kazi kwa Bidii zaidi na kuhakikisha Kuwa Almashauri ya wilaya ya Babati Inaongozwa Na Chadema

Katibu wa Wilaya ya Babati akitoa tathimini ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kati ya 2009 na 2014 katika wilaya yake, na kubainisha tumepanda kwa 40% katika uchaguzi wa mwaka jana 2014

Bi Ester Sarwat Akichangia agenda ya nini kifanyike kabla ya Uchaguzi mkuu wa October mwaka huu 2015



Wajumbe wa Wilaya ya Babati

Mwenyekiti wa Jimbo la Babati Mjini Mhe Mejor Madole akiwa kumbushia mambo ya kufanya kuelekea uchaguzi mkuu wa october ili kuweza kutayaarisha mazingira ya ushindi wa kishindo

Mwenyekiti wa Wilaya ya Babati Mhe Edward Mollel akizungumza na wajumbe walio jitikeza kwenye kikao cha tathimini katika wilaya yao, na kuwahasa kuwa wakumbuke uongozi ni wito katika kuwatumikia wananchi

No comments: