MWENYEKITI WA BAWACHA MKOA WA ARUSHA AMTEMBELEA MTOTO ALIYE ZALIWA AKIWA HANA SEHEMU YA HAJA KUBWA

Mwenyekiti wa BAWACHA moa waArusha Mhe Ceccy Ndossi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Arusha mjini Walitembelea Kata ya Sombetini na kukutana na Mwenyeji wao  Diwani wa Sombetini Mhe Ally Bananga, kwa Pamoja waliweza kufika kumuona mtoto ambaye amekuwa anateseka kwa Muda mrefu toka kuzaliwa kwake, Mtoto huyu alizaliwa bila ya kuwa na sehemu ya haja kubwa na hajawahi kufikishwa hospitali.

Mhe Ceccy amehaidi kumsaidia mtoto huyo kwa kumpeleka hospitali ili apatiwe  matibabu,pia wamejitokeza baadhi ya wasamaria wema ambao wameungana na Mhe Ceccy kumpatia mtoto huyu matibabu. 

Sehemu inayo onekana kwenye mwili wa mtoto ndio ambayo inatumika kwa sasa kama njia ya haja kubwa.


Mwenyekiti wa BAWACHA moa waArusha Mhe Ceccy Ndossi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Arusha mjini Mh Happy Charles pamoja na Diwani wa Sombetini Mhe Ally Bananga walipo wasili kumuona mtoto aliye kuwa akiteseka kutokana na uwezo wa wazazi kuwa duni





No comments: