Hapa
ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako maelfu ya wakazi wa
Shinyanga wamefurika katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mkuu ujao
wilaya ya Shinyanga hususani jimbo la Shinyanga Mjini.Mkutano huo
umeongozwa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ambaye ni
mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema ndugu Patrobas Katambi maarufu
kwa jina la "Mzimu wa Shelembi".
Viongozi
wengine machachari waliohudhuria mkutano huo ni mgombea ubunge kupitia
Chadema jimbo la Kahama mjini mheshimiwa James Lembeli,mgombea ubunge
jimbo la Kishapu Fred Mpendazoe na mgombea ubunge jimbo la Msalala
kupitia Chadema ndugu Paul Malaika.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog
Kadama Malunde, alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha 38,Angalia
hapa chini
Wakazi
wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la
Shinyanga
Makamanda wa Ukawa wakiwa meza kuu
Wagombea udiwani kupitia Ukawa katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga wakitambulishwa wakati wa mkutano huo
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano
Makamanda wa Ukawa na wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Mgombea
ubunge wa Chadema jimbo la Msalala Paul Malaika akizungumza na wakazi
wa Shinyanga ambapo alisema hata kama kuna mgombea mwenye sifa nzuri
ndani ya CCM wananchi wasimchague kutokana na kwamba mfumo mzima wa CCM
ni mbovu hivyo wafanye mabadiliko kwa kuiweka Ukawa madarakani
Mgombea
ubunge jimbo la Kishapu kupitia Ukawa ndugu Fred Mpendazoe akizungumza
na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka
watanzania kukubali mabadiliko kwani CCM imechoka huku akisisitiza kuwa
mgombea urais wa CCM John Magufuli hana kabila zaidi ya kabila la CCM
ambayo kamwe haiwezi kutoa rais bora
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti
wa Kamati ya Hamasa na Uenezi kanda ya ziwa Chadema Juma Protas
akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ambapo
aliwasisitiza wananchi kuchagua viongozi wa Ukawa ambayo ndiyo
mwarobaini wa maendeleo ya watanzania
Mgombea Ubunge jimbo la Kahama mjini James Lembeli akikaribishwa jukwaani kwa ajili ya kuzungumza na wakazi wa Shinyanga
Mgombea
ubunge wa jimbo la Kahama mjini mkoa wa Shinyanga wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia Ukawa James Lembeli akiuzngumza
katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kupuuza propaganda
inayoenezwa kuwa mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli kuwa ni msukuma
ili kuwarubuni watu wa kanda ya ziwa wampatie kura.
Lembeli
alisema hakubaliani na propaganda kuwa Magufuli kuwa ni msukuma hivyo
wasukuma wamuunge mkono kutokana na kutokuwa na msaada wowote kutetea
haki za wasukuma akitoa kuwa wakati akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge
iliyochunguza dhambi na shida waliyopatiwa wafugaji wakiwemo wasukuma
ambao waliuawa,waliteswa na kuibiwa mali zao ,Magufuli anayedaiwa kuwa
ni Msukuma hakufungua mdomo wake kutetea wafugaji/wasukuma dhidi ya
matatizo yaliyowakuta.
Wakazi wa Shinyanga wakimshangilia James Lembeli
Lembeli
aliongeza kuwa kutokana na kitendo hicho cha kukaa kimya dhidi ya
vitendo vya wafugaji hao inadhihirisha kuwa hayuko pamoja na wasukuma
hivyo asionewe huruma bali watanzania wamchague Edward Lowassa ambaye ni
jasiri na msema kweli.
Mheshimiwa
James Lembeli akimwombea kura mgombea urais wa Ukawa mheshimiwa Edward
Lowassa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa wakazi
wa Shinyanga
Lembeli
alitumia fursa hiyo kuwataka Wafuasi wa CCM wenye uchu wa kufanya
mabadiliko na kiu ya maendeleo wahamie Ukawa mara moja kwani kuna watu
ambao walikuwa na nguvu kubwa ndani ya CCM wamefanya maamuzi akiwemo
aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga baada ya kuchoshwa na
madudu ya CCM.
Mgombea
ubunge wa Chadema jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema pamoja na hujuma
anazofanyiwa na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa CCM akiwemo mgombea
ubunge wa CCM jimbo hilo Stephen Masele hatakata tamaa kuwapigania haki
wananchi na kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya wananchi
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Katambi
alizungumzia pia sakata la kutekwa kwake kisha kuchaniwa fomu zake za
ubunge sambamba na kufunguliwa mashtaka ya kupinga ubunge wake ambapo
alisema alipambana kuhakikisha kuwa jimbo hilo haliendi CCM na
atahakikisha kuwa CCM haishindi katika jimbo hilo
Katambi
alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Shinyanga kukubali mabadiliko na
hata ikitokea akafariki wakati mapambano ya kuiondoa CCM madarakani
yakiendelea wasikate tamaa wasonge mbele
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa Ukawa/Chadema
Mgombea
huyo wa ubunge wa Chadema katika jimbo la Shinyanga mjini Patrobas
Katambi amewataka wanaShinyanga kushikamana na kuepuka vitendo vya
usaliti na kuhakikisha kuwa wanawapa kura wagombea wa Ukawa badala ya
kushangilia pekee kwenye mikutano.
Mkutano unaendelea
Kulia
ni mgombea udiwani kata ya Shinyanga mjini atakayechuana na aliyekuwa
meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukaam(CCM) akitambulishwa
kwa wakazi wa Shinyanga
Mheshimiwa
James Lembeli na fimbo yake ya kimila akimsikiliza kwa umakini zaidi
mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Mkutano unaendelea
Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas akizungumza katika mkutano huo
Wananchi
wakiwa wamenyoosha mikono baada ya kuulizwa kama wako tayari kuleta
mabadiliko katika jimbo la Shinyanga mjini na nchi kwa ujumla
Katambi
akizungumza na wakazi wa Shinyanga leo ambpo alivitaja baadhi ya
vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kilimo na ufugaji,viwanda,kupambana na
umaskini,ujinga na malazi..
No comments:
Post a Comment