TAARIFA KWA UMMA/WADAU




MKUTANO WA WADAU WA CHADEMA WAPENDA MABADILIKO NA UHURU WA KWELI.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kinapenda kuwatangazia na kuujulisha umma na wadau wote kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kuwa tarehe 14/02/2015 katika JIJI la Arusha yalipo makao makuu ya chama kwa kanda, kuwa kutafanyika mkutano wa Wadau.
Wadau hawa ni pamoja na wanasheria wote, wachumi, wahasibu, wahandisi, wahadhiri wa vyuo na waalimu, wanahabari, wafanyabiashara, viongozi wa dini na makundi yote maalumu na ya kitaaluma, wote wanaalikwa kushiriki katika mkutano huu ambao una lengo la kutoa fursa kwao kama watanzania wakiwa kama wadau wa kweli waweze kuitumikia nchi yao kupitia CHADEMA.
Katika mkutano huu wadau watapata fursa ya kushirikishwa katika nafasi za kimaamuzi na kiutendaji za kanda kwa lengo la kuijenga na kuiimarisha CHADEMA ambayo imekuwa na imeendelea kuwa tumaini kwa Watanzania kwa wakati huu wa uhitaji mkubwa wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.
Mkutano huu utafunguliwa na pia kuhudhuriwa Mwenyekiti wa CHAMA Taifa Mhe Freeman Mbowe (MB) ambaye pia ni mbunge kutoka Kanda ya Kaskazini pamoja na viongozi wengine wa kitaifa.
TAARIFA YA UKUMBI TUTAENDELEA KUWAPA KADRI JINSI MAMBO YANAVYOZIDI KWENDA.
Wadau wote mnakaribishwa sana kuhudhuria mkutano huu.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ushiriki kwenye mkutano huu tafadhali tumia mawasiliano kwa njia zifuatazo:
Simu: +255 758 976 260
+255 656 557 586
+255 755 282 878
Barua pepe: chademakaskazini@gmail.com
chademakaskizinidata@gmail.com
Amani S. Golugwa
KATIBU – KANDA YA KASKAZINI

No comments: