MBOWE APONGEZA KIWANDA CHA KIBO NATURAL WATER BAADA YA KUFANYA ZIARA KIWANDANI HAPO

Mh Mbowe akipata  Maelezo ya baadhi ya bidhaa zizalishwazo na Kiwanda cha Kibo Natural Water

Mbunge wa jimbo la Hai na Mwenyekiti wa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Freeman Mbowe leo Jumanne 19/ 07/2016 amefanya ziara katika kiwanda cha maji cha Kibo Natural Water  kilichopo Shari Bwani Machame mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo ameongozana na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Hai, Mhe. James Mushi.

Akiwa katika ziara hiyo Mbowe amepongeza sana uongozi na wazo zima la kufungua Kiwanda hicho katika Wilaya ya Hai, kiwanda kitasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Hai, kuongeza kipato kwa wakazi waishio Hai na kuongeza pato kwa Taifa kiujumla pamoja na kutoa nafasi za ajira kwa wakazi wa eneo hilo.

Akiongea baada ya kumaliza ziara hiyo Mhe. Mbowe ameendelea kuwapongeza na amewataka kama kuna tatizo lolote milango ipo wazi kwani yeye ndiye Mbunge wao yupo tayari kushirikiana nao katika kuleta Maendeleo katika Wilaya ya Hai.


Mh Mbowe kwenye picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda cha Kibo Natural Water

Mh Mbowe akisalimiana na Mtoto wakati akiwa kwenye Ziara ya Kukitembelea Kiwanda cha Kibo Natural Water

Mh Mbowe akisaini kitabu cha Wageni katika Kiwanda cha KIbo Natural Water

No comments: