WADAU WAUNGANA NA MBOWE KUMALIZIA UJENZI WA BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA HARAMBEE MACHAME



Mbunge wa jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe, katika kuhakikisha anapata Shilingi Milioni 50, kumalizia ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari Harambee iliyopo Nshara Machame Mkoani Kilimanjaro, Mbowe amekutana na wadau mbalimbali na wamekubali kuungana nae kuhakikisha bweni hilo linakamilika kabla ya tarehe 30/7/2016.

Bweni hilo lenye ghorofa moja likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 120, na wanafunzi 181 ambao wana sifa za kuendelea na kidato cha V na VI lakini wamekosa nafasi ya kuendelea, wanafunzi 81 wataandikishwa katika shule ya Sekondari Harambee.

Sera ya serikali inataka shule ili iwe na kidato cha V na VI lazima iwe na bweni, hivyo bweni hilo lazima likamilike kabla ya muda wa mwisho wa wanafunzi kuanza masomo.



Wadau ambao wamemshika mkono na kuchangia bidhaa, vifaa vya ujenzi na wengine pesa ni pamoja na Bw. Harold Shoo, Benjamin Mengi, Kanali Mstaafu Muro, Yusuf Hussein (Kley).

Mbowe amewataka wadau zaidi kujitokeza kusaidia ujenzi huo ili uende kwa haraka na kumalizika ili wanafunzi 81 waanze masomo kwa haraka na wengine 61 waliobaki watachomekwa kwenye shule nyingine ili waweze kuendelea na masomo .

Wanafunzi 181 ni wengi sana wasipokwenda shule, taifa litakosa watu wazalishaji wenye kuleta ushindani katika soko la ajira kwa kuzalisha bidhaa na kutoa huduma zenye ubora wa kimataifa.




No comments: