MBUNGE WA KARATU NA WENZAKE WAHOJIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA


Mh Ceccilia Paresso Mbunge wa Viti Maalumu  (Kushoto),Katibu wa Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa ArushaMh Amani,Mbunge wa Karatu Mh Willy Qambalo ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu Mh Jublate Mnyenye ( Kulia) Na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu (Nyuma) Wakiwasili  Central Polisi Arusha Mapema Leo Tarehe 27/07/2016

Leo Mbunge wa Karatu Mh Willy Qambalo akiambatana na Mh Ceccilia Paresso Mbunge wa Viti maalum Koa wa Arusha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu Mh Jublate Mnyenye na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu Mh Bajuta walifika Central Polisi Arusha Kufuatia Wito wa Jeshi la Polisi kutokana na  kunfanya Mkutano wa tarehe 23/07/2016,Mkutano huo haukuwa wa Kisiasa bali wa Kimaendeleo
 Hivyo leo Majira ya Saa tano Asubuhi walikifa wakiwa wamefuatana na Katibu wa Kanda na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa pamoja na Viongozi wengine wa Chama.
Wote walioitwa na Jeshi la Polisi wamefanikiwa kuhojiwa kila mmoja na ametoa maelezo yake na kuondoka.Mahojiano hayo yalichukua takribani masaa 3.





No comments: