ZIARA YA KATIBU WA BAVICHA MKOA WA ARUSHA WILAYANI NGORONGORO.



Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Arusha Kamanda Jenipher Mwasha katika picha ya pamoja na Makamanda wa Msingi wa Sanjan Katika Kata ya Ngarasero,


Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Arusha Kamanda Jenipher Mwasha ambaye ameambatana na Kamanda Ayubu Issangya katika Ziara yake Wilayani Ngorongoro ambayo leo imeingia Siku ya Tano(5).
Ziara hii ilianzia katika Tarafa ya NGORONGORO ambako alifanikiwa kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Ngazi ya Wilaya na Ngazi ya Kata waliopo katika tarafa hii, pia alifanikiwa kufungua Msingi Mmoja katika Kwenye Kijiji cha Oloirobi,Kata ya Ngorongoro .

Kisha ameendelea na Ziara yake katika Tarafa ya Sale ambako nako alifanikiwa kutoa mafunzo ya Ujezni wa Chama kwa kuwajengea uwezo Viongozi Wa Kata Nne (4) zilizopo katika Tarafa hii, pia aliwapa mafunzo juu ya uundaji wa Misingi ambapo baada ya mafuzo hayo Kamanda Jenipher Mwasha alifanikiwa kufungua Misingi Sita(6) Katika Maeneo tofauti katika Tarafa hii ya SALE. Misingi iliyofunguliwa ni Msingi wa Madukani katika Kata ya Sale, Msingi wa Msurumuni Katika Kata ya Piyaya, Msingi wa Sanjan Katika Kata ya Ngarasero, na Misingi ya Ngabola, ,Oljoro, Mbetesi katika kata ya Samunge.

Leo anaendelea na Ziara yake Katika Tarafa ya WASO ambapo ataendelea na mafunzo na kuzindua Misingi.

Kamanda Jenipher akiendelea na Mafunzo ya Ujenzi wa Chama katika Kata ya Sale

Kamanda Jenipher Akizindua Msingi Katika Kata ya Piyaya

Kamanda Jenipher akizindua Msingi katika Kata ya Samunge

Kamanda Jenipher Akizindua Msingi Katika Kata ya Ngarasero


No comments: