Mwenyekiti
wa Arusha Development Foundation Mr. Elifuraha Paul Mtowe.
|
Leo tunakabidhi eneo la Ujenzi wa Hospitali
ya Mama na Mtoto kwa Maternity Africa,
Maternity Africa ni Taasisi Huru inayoshughulika
na uzazi bora na Afya ya Mama na Mtoto wakati wakujifungua, Taasisi hii iko Afrika
Nzima na ina hospitali katikaNchi mbali mbali za Africa.
Taasisi hii inaongozwa na moja ya Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake Duniani Dr. Andrew James Browning na yeye mwenyewe
pamoja na Taasisi yake ndio watakaosimamia ujenzi wa Hospitali hii na kuendesha.
Hospitali itakayojengwa hapa ni ya kutoa
huduma ya Mama na Mtoto wakati wakujifungua na Chuo cha kufundisha Wakunga kwa ajili
yakusaidia huduma kwa Mama na Mtoto wakati wakujifungua, wakunga hawa watatoka katika
vituo vyote vya Afya katika Jimbo la Arusha na maeneo mengine ya Nchi.
Hospitali hii itakuwa ndio hospitali ya
kwanza itakayotoa huduma kwa Mama na Mtoto tu ambayo pia itakuwa na chuo cha kufundisha
wakunga mbinu bora na za kisasa zitakazoendana na hali ya kina Mama wa Tanzania
wakati wa maandalizi ya uzazi na hata kujifungua.
Hospitali hii itakuwa ni ya kisasa na yenye
vifaa vya kisasa na itajengwa kwa gharama ya Dola Milioni Tatu na Nukta Mbili sawa
na Shilingi Bilioni Sita, NuktaTano Sita za Kitanzania kwa thamani ya sasa ya shilingi.
Wakina Mama watakao hudumiwa hapa ni kutoka
sehemu yoyote ya Tanzania, lakini ni lazima waanze kupata huduma za awali hapa kabla
ya kujifungua, aidha kutakuwa na kitengo maalum cha kuwafuatilia wakina Mama
ambao wako nje ya Arusha wenye kuonyesha matatizo wakati wa ujauzito na kutakuwa
na magari maalumu ya kwenda kuwachukuwa kuwaleta Kliniki na hata kwenda kuwachukua
baada ya kupata taarifa za kuanza dalili za kujifungua na hata kuwarudisha nyumbani
baadaya kujifungua.
Kwa kesi maalum wakina Mama wenye kuhitaji
uangalizi maalum watalazwa hapa mpaka watakapojifungua na baada ya kuthibitishwa
kuwa wako salama ndipo watakaporudishwa majumbani.
Huduma zote hizi zitakuwa ni bure, toka wakati
wa huduma za Kliniki, Kufuatwa Nyumbani, kujifungua na Kurudishwa nyumbani baada
ya kujifungua.
Aidha kutakuwa na kitengo maalum kwa ajili
ya Matibabu ya Festula ambacho pia kitatoa huduma bure kwa wakina Mama wote watakao
kuwa na tatizo hilo.
Tuna amini idadi kubwa ya kina Mama
watajifungua hapa na wote watajifungua salama na watapewa huduma bora na sawa kwa
kila mtu na Hospitali hii haitakuwa ni kwaajili ya wanawake wasio na uwezo tu itakuwa
ni kwa ajili ya wanawake wote.
Nimesimama hapa nikiwa nina furaha mimi kama
Mwenyekiti wa Arusha Development Foundation nikiwa nimeweza kutimiza ombi la
Mheshimi wa Mbunge mara baada ya Kupata Ubungealipoiagiza Taasisi na Mimi Mwenyewe kuwa anataka kuona kuwa tunafanikiwa
kuwa na hospitali ya Mama na Mtoto. Lakini pia Rafiki yetu Hayati Wakili Nyaga Mawala
alisema “..sitaki kingine chochote katika eneo hili nataka Hospitali ya Mama na
Mtoto “ Leo hii niko hapa mbele yenu Maternity Africa na wageni
waalikwa kushuhudia utekelezaji wa Upendo huu mkuu .. lakini pia Kiongozi w aKambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni Mh. Mbunge Freemani Aikael Mbowe tukiwa kwenye mazishi ya Rafiki yetu Wakili
Nyaga Mawala Jijini Nairobi alisema , hakikisheni
mnajenga Hospitali ya Mama naMtoto kama mlivyo tamani pamoja naNyaga.
Jina la Hospitali hii litakuwa “Mama na Mtoto” Ujenzi wa Hospitali hii utachukuwa
miaka mitatu toka utakapoanza na utaanza mara moja baada ya taratibu za vibali vya
ujenzi na michoro kukamilika. Fedha zimeshapatikana.
Mawakili wa ArDF; Mawala Advocates wametushauri
vyema na leo hii tunaweka sahihi makabidhiano haya ya eneo hili tukiwa tumeangalia
mambo yote muhimu ya kisheria, muda wakujenga na ubora wa hospitali na wako hapa
kuhakikisha tukio hili la ujenzi wa hospitali linaanza.
ArDF tunawashukuru sana Maternity Africa
kwa Upendo wao , kwa mujibu wa taarifaya
Wizara ya Afya, ripoti ya vifo vya kina Mama
kati ya mwaka 1992 hadi mwaka jana 2014 inaonyesha vifo vya kina Mama
vinavyotokea wakati wa kujifungua vimepungua kwa asilimia 14 tu hivyo hali katika
nchi bado ni mbaya.
Katika hospitali ya Mt. Meru hapa Arusha
idadi ya akina Mama elfu moja hujifungua kila mwezi na muda wote vitanda vya wodi
yao huwa vimejaa wakisubiri kujifungua na wengine wakiwa wamelazwa chini hivyo Hospitali
hii itasaidia kupunguza mzigo kwa Hospitali ya Mt. Meru namaumivu kwaMtoto na
Mama wa Tanzania .Hivyo ni wito wangu kwa Serikali kuwa sasa Maternity Africa wanapaswa kuungwa mkono na kila ofisi na
kila mtaalamu ili kufanikisha ujenziwa Hospitali hii mapema.
Ninapenda kuishukuru kama tituliyoiunda ya
Madaktari bingwa wa hapa Arusha ili kutushauri kuhusu nia yetu ya Ujenzi wa Hospitali
hii kwa mchango wao wahali na mali ilikufanikisha jambo hili, tunakushukuru sana
Dr. Msuya wa St. Thomas, Dr. Aziz Msuya aliyekuwa Daktari Mkuu wa Hospitali ya Wilaya
ya Meru, sasa hivi yuko Hospitali ya Mkoa wa Kinondoni, Muuguzi Mwandamizi Mkuu
wa CEDHA Dada Ndeki, Dokta Makando wa St. Thomas na Dokta Lekundayo wa Mount
Meru Hospital , bila kumsahau Happy Mwamasika dada yetu ambaye jitihada zake katika
ndoto hii nidhahiri na za kushukuriwa.
Kwa dhati kabisa namshukuru Mbunge wa Jimbo
la Arusha Mjini Mh. Godbless Jonathan Lema kwa maono yake na roho yake isiyochoka
dhidi ya anachokiamini licha ya kukatishwa tama mara nyingi kuhusu jambo hili.
Pia nampa pole mke wake Neema Godbless Lema
kwa kuhusishwa na eneo hili kuwa alikuwa amemilikishwa kinyemela, nafahamu alivyoandikwa
vibaya kwenye vyomba mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uzushi
huo, hata hivyo hapana shaka kuwa maumivu hayo yanathibitisha kwamba kazi yashetani
ni kuharibu, kuchinja na kuua. Tunafuraha sana leo sisi ArDF kuwa tumemshinda shetani
na sasa tunakabidhi eneo hili rasmi kwa Maternity Africa ili ujenzi wa Hospitaliya
Mama na Mtoto na chuo cha Wakunga uanze.
Maternity Africa tunawashukuru sana kwa upendo
wenu wa Mama na Mtoto wa Africa, Mungu awabariki sana.
Mwenyekiti
Arusha
Development Foundation.
Mr.
Elifuraha Paul Mtowe.
No comments:
Post a Comment