Mbuge wa Arusha Mjini Mhe Godbless J.Lema |
Mwaka 2010 wakati
naomba kuchaguliwa kuwa Mbunge moja ya
ahadi zangu kubwa kwa Wananchi ilikuwa
ni kujenga Hospitali ya Mama na Mtoto .Ndoto hii ilitokana na ukweli kwamba bado matibabu yanayohusu
Mama na Mtoto katika Bara lote la Afrika
ni yakusikitisha sana .
Tanzania ni miongoni
mwa Nchi ambazo matatizo ya Afya kwa ujumla yana mgogoro mkubwa hususani katika
afya ya Mama na Mtoto. Taarifa za Vifo za kina Mama mpaka mwishoni mwa mwaka
2010 zilikuwa ni vifo Elfu Saba na Mia Tano, sawa na wastani wa vifo Mia Sita
Ishirini na Tano kwa mwezi, sawa na vifo Ishirini na Moja kwa siku, (kwa mujibu
wa taarifa za Wizara ya afya TZ) , hali hii ilitufanya Mimi na Rafiki zangu kufikiria namna ya kumsaidia Mama anayejifungua na Mtoto anayezaliwa .
Pamoja na mambo mengine
ambayo taasisi hii inayafanya na inaendelea kuyafanya tuliweka lengo mathubuti kwa ajili ya afya ya Mama na Mtoto . Tulianza
juhudi za kutafuta na eneo kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Mama na Mtoto ,
kazi hii haikuwa rahisi hata kidogo , katika kuendelea kuangaika kwa ajili ya
jambo hili muhimu tulikutana na Kaka yetu na Rafiki yetu Mpendwa sana Hayati
Wakili Nyaga Mawalla .
Nyaga alikuwa Mtu mzuri
, mwenye mawazo chanya, Mzalendo , na mwenye Upendo na rafiki zake na maendeleo
. Tulimweleza mawazo yetu juu ya afya ya Mama na Mtoto na changamoto tuliyokuwa
nayo ya jinsi ya kutekeleza Ndoto hii nzuri .
Tunaikumbuka siku ile ,
kwani mwisho wa kikao chetu Hayati Wakili Nyaga Mawalla alitoa eneo la kujenga
Hospitali ya Mama na Mtoto na ahadi ya kugharamia michoro ya ujenzi wa
Hospitali hiyo pindi tutakapokuwa tayari kuanza ujenzi.
Leo tuko hapa na yeye
hayupo tulitamani angekuwepo hapa leo aone jinsi nia yake njema inavyotekelezwa kwa faida kubwa ambayo ni Utu ,Upendo ,na Huruma . Our Brother
Nyaga your presence is not here with us today but your good heart will never be forgotten
to us and to our society.
Hata hivyo ,tumekutana
na changamoto nyingi katika safari hii , uongo mwingi , kashfa nyingi na
dhihaka zenye lengo la kutuvunja moyo , wapo waliosema eneo hili limeuzwa na leo tunasema Hospitali
inaanza kujengwa .
Taarifa ya WHO ya
mwisho wa mwaka huu (2015) inaonyesha katika kila Wanawake Laki Moja
wanaojifungua Wanawake 410 hufariki kwa kukosa huduma nzuri wakati wa kujifungua hapa Tanzania , kwetu
sisi hii ni changamoto na kushindwa ni
falsafa iliyopeteza maana , Maisha ya
Mama na Mtoto yana muhitaji kila mmoja wetu.
Nawashukuru sana
Maternity Africa na marafiki zenu , Nia yenu njema kwa Binadamu Duniani imedhihirika leo kwa Mama na Mtoto wa Arusha . Mama Teresa aliwahi kusema “The greatest science in the world, in
heaven and on earth is LOVE”
Moyo wangu umejaa
furaha sana leo nawashukuru sana Wakurugenzi wote wa ArDF, Mawalla Trust Ltd na Watu wote ambao mmekuwa msaada katika jambo
hili hadhimu .
Mungu awabariki sana .
Godbless J
Lema ( MB)
No comments:
Post a Comment