MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri
wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson
Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa Juni 29 mkoani Kagera.
Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio
na Mwanahalisi online ,Edson
Kamukara wamesema ni pigo kwa tasnia ya
habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya
uandishi wa habari.
“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi
kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa
wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbowe
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi
amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia
misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
“Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri
kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema
Mengi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama
hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson
Kamukara katika viwanja vya Leaders Club
Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki
(katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama
hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson
Kamukara katika viwanja vya Leaders Club
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Hali
Halisi Publisher wachapishaji wa Mawio na Mwanahalisi Online,Sued Kubenea
wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana
mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa
Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. |
Sehemu ya waombolezaji wa kuaga mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. |
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akitoa hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. |
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akitoa hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. |
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media
wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari wakiwa katika huzuni wakati
wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe akitoa hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. |
Kila aliyesimama kuzungumza aliishia
kuangusha chozi; wakikumbuka kazi nzuri iliyofanywa na Kamukara, mmoja
wa wandishi wa habari mahiri nchini.
Kamukara aliyefariki dunia katika mazingira yaliyosheheni utata, Alhamisi 25 Juni mwaka huu, nyumbani kwake, Mabibo jijini Dar es Salaam, anatarajiwa kuzikwa Jumatatu wiki ijayo, nyumbani kwao Muleba, mkoani Kagera.
Miongoni mwa waliofika kutoa heshima za
mwisho kwa Kamukara, ni pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa
Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Reginald Mengi na mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe.
Wengine, ni Mbunge wa Bukoba Mjini,
Balozi Khamis Sued Kagasheki; Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod
Slaa; Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Nevile Meen.
Meena alisema, Kamukara ni miongoni mwa
waandishi wa habari wa chache nchini, wanaofanya kazi zao kwa uadilifu
na kufuata miiko ya uandishi.
“Sisi katika vyombo vya habari, tulikuwa
tunamuona Kamukara kama mtu ambaye anaweza kukabidhiwa jukumu kubwa la
kuongoza chombo cha habari siku zijazo. Lakini leo, mwenzetu huyu
ametangulia mbele ya haki. Ni vema tukamuenzi kwa kufuata nyayo zake,”
ameeleza Meena.
Amesema, tasnia ya habari imempoteza mtu jasiri na aliyekuwa na weledi mkubwa katika utendaji wake wa kazi.
“Tumepoteza mtu jasiri, mahiri, asiyedanganyika na mwenye msimamo imara katika kazi yake,” alisisitiza Meena.
Naye Mbowe alisema, maslahi
ya waandishi wa habari nchini, ni duni sana. Waandishi wengi hawana bima
ambazo zingesaidia familia zao.
Amesema, “Nichukue nafasi hii, hasa kwa
kuwa hapa yupo mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi, nitoe ombi kwa
wamiliki wa vyombo vya habari, tuweke utaratibu wa kuwawekea bima ili
iweze kusaidia waandishi.”
Mbowe amesema, umuhimu wa kuwa na bima ni
mkubwa kwa kuwa “maslahi ya waandishi ni madogo.” Amesema, ikiwa
waandishi watawekewa bima, itawasaidia kuendesha familia zao, pale
wanapokutwa na mauti.
Akimzungumzia Kamukara, Mbowe alisema, “Edson (Kamukara), alikuwa mwandishi wa habari asiyetegemea bahasha.”
Amesema, “…alikuwa mkweli, mwadilifu na mchapa kazi. Ni vema waandishi wakamuenzi kwa kufuata matendo yake.”
Kwa upande wake, Mengi aliwataka
waandishi wa habari kusimamia maadili katika uandishi wao, ikiwa ni
pamoja na kuepuka rushwa kama alivyokuwa Kamukara.
Amesema, “Mimi sitaki kutafuna maneno.
Kamukara amekufa wakati akifuatilia habari moja kubwa. Katika siku za
hivi karibuni, alikataa mamilioni ya pesa ambayo aliahidiwa kama
angeacha kuchunguza kuandika habari hiyo, lakini yeye alikataa kupokea
pesa hizo na akaandika habari na kuitoa.”
Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP amesema, waandishi hawapasi kuendekeza rushwa katika kazi zao.
“Rushwa ni tabia ya mtu, sio kwamba ukiwa na kipato kidogo ndio sababu ya kupokea rushwa.”
Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), Balozi Kagasheki amesema, amemfahamu Kamukara kutokana na ushujaa wake kwenye tasnia ya uandishi.
Amesema, sifa na ujasiri wa Kamukara
tayari umezungumzwa na watu waliotangulia na kwamba, kinachopaswa ni
kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amuweke pema.
Naye Kubenea alisema, kampuni ambayo imekuwa mwajiri wa Edson Kamukara kwa miezi minne na siku tatu sasa – HHPLimited – “imepata pigo.”
Amesema, “Ni masikitiko makubwa. Ni
uchungu usio na kiwango. Ni ukiwa usiozibika. Tumeondokewa na ndugu.
Tumeondokewa na rafiki. Lakini zaidi, tumeondokewa na mchapapakazi.
Tulimpenda sana Edson. Tuseme kweli; naye alitupenda.”
Amesema, “Tulifanya naye kazi kwa
uelewano mkubwa. Tulithamini mawazo yake kama yeye alivyothamini ya kila
mmoja wetu. Kwa hakika, tutamkosa na pengo ambalo ametuachia, haliwezi
kuzibika.”
Kubenea ambaye mara kwa mara hotuba yake
ilikuwa inakatizwa na kilio, aliwashukuru wote walioungana na kampuni
yake katika msiba huo mkubwa.
No comments:
Post a Comment