Mh Freeman Mbowe Akitazama mazingira ya Shule ya Sekondari ya Harambee Nshara |
Mbunge wa jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe amehakikisha kusimamia ujenzi wa bweni la shule ya Sekondari ya Haramabee iliyopo Nshara Machame mkoani Kilimanjaro kwa kuhakikisha ujenzi unakamilika na kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 ambao wana vigezo vya kuendelea lakini wamekosa nafasi.
Katika jitihada za kuifanya shule ya Sekondari ya Harambee kuwa mfano Hai, Mhe. Mbowe amesema watahamishia nguvu katika shule nyingine kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo Waheshimiwa Madiwani, Wananchi kuzifanya shule za Wilaya ya Hai kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini.
Idadi ya wanafunzi wenye sifa lakini wamekosa shule ni 181, baada ya kukamilika kwa bweni hilo wanafunzi wa kike na kiume 120 watapa nafasi katika shule hiyo na wengine 61 watatafutiwa nafasi katika shule nyingine.
Mhe. Mbowe amefanya ziara hiyo akiongozana na Meya wa mji mdogo wa Hai, Mhe. Nesefort Shayo, Afisa elimu wa wilaya, Bw. Juges Kakyama, Diwani wa Kata ya Machame Mashariki, Mhe. Clement Kwayu, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai, Mhe. James Mushi wakiwa na mwenyeji wao Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Harambee, Bi. Florence Muhochi.
Kutokana na sera ya Serikali kuagiza ili shule iweze kuwa na kidato cha 5 na 6 lazima iwe na bweni (Dormitory), Mhe. Mbowe ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali na Madiwani wa jimbo la Hai kuhakikisha bweni hilo linakamilika kabla siku ya mwisho ya wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 kuandikishwa kuanza masomo.
Mhe. Mbowe amesema anataka shule ya Sekondari ya Harambee iwe mfano, kwa kuweka nguvu pia kumalizia ujenzi wa nyumba ya mwalimu iliyopo shuleni hapo ambayo ilianza kujengwa 2007, kuweka maktaba katika hali nzuri pamoja kuongeza madarasa mawili, kupiga rangi majengo na kutengeneza sehemu ya kulia (dinning).
Mhe. Mbowe amesema ataanzisha program ya kuwashirikisha wanafunzi waliosoma katika shule hiyo (Lumnia program) popote walipo nchini waweze kushiriki kuifanya shule yao kuwa mfano wakishirikiana na Mbunge wao wa jimbo la Hai.
Mhe. Mbowe ameomba baada ya bweni hilo kukamilika, kwa kuwa shule ya Harambee itachukua watoto 120, na kwa kuwa sera ya serikali inataka wanafunzi watoke nchi nzima, sio kitu kibaya lakini amemuomba Afisa elimu wa Wilaya kwamba nusu ya watoto watoke Hai na nusu watoke maeneo mengine hapa nchini.Jumla ya wanafunzi 680 kutoka Wilaya wamepata shule, waliobaki 181, Mhe. Mbowe amejitoa kuwahangaikia wapate shule, kwa kukamilisha bweni hill kabla ya tarehe 30/7/2016, watoto 181 wasipokwenda shule ni hatari kwa Taifa tunalolijenga pindi tutakapohitaji watu wazalishe bidhaa na kutoa huduma katika dunia ya sasa ya ushindani.
"Kwa kuwa bweni hilo limejengwa kwa nguvu za wananchi wa Hai hadi hapo lilipofikia na mimi kama Mbunge wa Hai siwezi kukubali kuona wanafunzi 181 wanakosa elimu kwa sababu ya kukosekana bweni, pia lazima wakazi wapewe kipaumbele kwanza, ndipo watu wa nje ya Hai wapewe nafasi ni vizuri wanafunzi wetu wakachanganyikana na watoto wa maeneo tofauti tofauti ili kujuana na kujenga mahusiano mema na kujua tamaduni mbalimbali za watu wengine" amesema Mbowe
Wilaya ya Hai imefanikiwa kuwa na shule kila kijiji, ingawa sera ya Serikali inataka kila Kata iwe na shule, hii ni hatua kubwa ya kimaendeleo ambayo imefanywa katika jimbo la Hai ambalo linaongozwa na Mbunge, Freeman Mbowe.
Picha ya Mh Mbowe na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Harambee Nshara |
Mh Mbowe akiteta jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Harambee Nshara |
1 comment:
Online Casino | Nagara - Nagara - Agen SBOBET
Online Casino with Free 1xbet Spins No Deposit 온카지노 for all new players! Latest promotions, latest bonuses and promotions at Agen 메리트카지노 SBOBET!
Post a Comment